Yawakera bidii yangu
Yawasuta Nafsi yangu
Ulaghai mliojilimbikizia
Kwa ahadi za kinafiki
Sio penzi langu niyakumbuke
Ila yenu Hila yabidi nijichunge
Werevu wenu ushawaaribikia
Maisha yangu nakudodoa we abiria
Nashukuru kwa Muda wote
Kwa ufala ulionifikiriria
Na kiapo naaapa sasa
Adui Utakoma.
Ulaghai wako do laana yako
Uovu wako do baraka zako
Tusizoeane na Uoze uozeane
Kaburi la sahau nishakutinga.
Simu zangu kelele sasa
Shida zangu Kicheko kwako
Hujuma iliyoje
Urafiki kugeuka unafiki